Monday, May 22, 2017

Madhara ya Chai na Kahawa Kiafya

CAFFEINA/KAFEINA.

Kafeina ni nini?:

1. Kafeina ni madawa ya kulevya kundi la ‘Stimulants drugs’.
Utashangaa. Habari ndiyo hiyo. Hii ndiyo sababu kwa mtu aliyezoea kunywa chai hii kila siku au kahawa, siku asipokunywa kichwa humuuma, ni kwa sababu amekuwa mtegemezi au teja wa kafeina.

Kafeina ni kiungo mhimu karibu katika soda zote zenye rangi nyeusi; Coca-cola, Pepsi, Sayona nyeusi, Azam cola na kadharika. Kafeina huongezwa pia katika Red bull, Malta na katika baadhi ya dawa za kupunguza maumivu mwilini.

Kwahiyo Kafeina ambayo hupatikana katika chai na kahawa ni aina mojawapo ya madawa ya kulevya.

2. Kafeina ni kikojoshi (diuretics).
Kafeina ni dawa ya kukufanya ukojowe. Ukinywa kikombe kimoja cha kinywaji chenye kafeina yaani chai au kahawa, basi muda si mrefu utaenda kukojoa vikombe viwili. Kwa sababu kafeina ni taka isiyotakiwa mwilini, mwili utafanya kila uwezalo ikibidi ujikamuwe wenyewe kupata maji ya ziada kuweza kuitoa kafeina hii uliyoinywa kwa kisingizio cha chai, kahawa au soda.

Madhara yake ni nini?, Moja; kama unakunywa kinywaji na muda si mrefu unalazimika kwenda kukitoa inamaanisha kinywaji hicho hakikutumika vema na mwili. Pili; kumbuka ulikunywa kikombe kimoja na umeenda kutoa viwili, hivyo umekopwa maji mwilini mwako na ukumbuke kuwa MAJI NI UHAI.

3. Kafeina husababisha KANSA.
Seli ndani ya mwili lazima zibaki katika kiasi kidogo cha alkalini kutoka 7.2 mpaka 7.4, wakati 7.0 ni ya kati au husemwa sifuri katika kipimo cha PH (potential hydrogen). Chini ya 7.0 ni asidi na juu ya 7.0 ni alkalini. Kafeina yenyewe ni asidi, hivyo ikiwa mtu anafanya chai au kahawa ndivyo vinywaji vyake vya kila siku basi mtu huyo lazima atakuja kupatwa na kansa katika siku za usoni kwakuwa seli za kansa huishi katika hali ya uasidi pekee na kafeina ndimo mazingira mazuri ya kuishi asidi.

Jarida moja la afya la Uingereza, ‘The British Medical Journal Lancet’, limeripoti uhusiano mkubwa uliopo baina ya utumiaji wa kahawa na kansa ya kibofu cha mkojo na kupungua kwa uzarishwaji wa mkojo.

4. Kaffeina huchangia upotevu wa madini na vitamin mhimu mwilini.
Kafeina ambayo ni kikojoshi, huyalazimisha maji kukimbia nje ya mwili kwa haraka na kuziacha seli bila muda wa kutosha kuyatumia maji hayo, maji yanapokimbia kwa haraka nje ya mwili huyakimbiza pia madini mhimu nje ya miili yetu.

5. Kaffeina husababisha kisukari.
Mwili una vyanzo 3 vya nguvu ambavyo ni Sukari, Mafuta, na Maji/Chumvi. Tumesema kaffeina ni kikojoshi, hivyo kaffeina hupelekea upotevu usio wa lazima wa maji mwilini, mwili unapokosa maji kama chanzo chake cha nguvu, moja kwa moja huhamia kuitegemea sukari kama chanzo chake cha nguvu na mwishowe kisukari lazima kitokee.

6. Uchovu sugu.
Wapenzi wengi wa chai ya rangi na kahawa mara nyingi wanapojisikia uchovu hukimbilia kikombe cha kahawa au chai. Kaffeina iliyomo katika chai au kahawa huenda kuiamsha na kuitumia nguvu iliyokuwa imehifadhiwa na mwili kwa ajili ya matendo ya dharura na kukuacha wewe ukiwa huna nguvu ya ziada kwa ajili ya kazi za dharura, matokeo yake ni mwili unakuwa upo katika hali ya msukosuko muda wote.

Utolewaji wa sukari iliyokuwa imehifadhiwa, kunapelekea mfadhaiko mkubwa kwenye mfumo wa dharura wa mwili. Unaposhitushwa kidogo tu, unakuwa na nguvu za haraka (Unahamaki) kushughurika na tatizo. Hali hii hatimaye inaweza kupelekea kukauka kwa tezi ya adreno kutakakosababisha damu chache yenye sukari (hypoglycemia), udhaifu, na kuumwa sana iwapo sukari haitachukuliwa mapema kupandisha juu damu sukari.

Kwa sababu ya biashara kuunda vyakula vyetu vyote maalumu na vinywaji vyenye radha mpya, radha nzuri na nguvu ya kutosha kwa kutumia kafeina toka katika mimea na mitishamba kama vile ginseng kuisisimua tezi ya adreno, kunasababisha Ini kutoa sukari iliyokuwa imehifadhiwa mwilini kwa ajili ya matumizi yake ya dharura.

Hakuna nguvu iliyomo kwenye kafeina au ginseng. Kuna majina mengine mengi ya visisimuwaji hivi kama vile, kokwa za guru, kokwa za cola na mfalme wa yote ni guarana. Mbegu za guarana zina kiasi cha kafeina mara tatu zaidi ya zile za kahawa, na hawatakiwi kuliorodhesha neno kafeina kwenye vifungashio (packages) au kontena.

Ungaunga wa guarana hutumika kutengenezea vidonge vya kupunguza uzito kwa sababu kafeina itazisambaratisha hisia za njaa, lakini hakuna mahala neno kafeina linaonekana kwenye vifungashio vya dawa hizi.

Kuna mimea, kokwa na kemikali nyingi ambazo zitaisisimua tezi ya adreno na kusababisha ini kuitoa sukari iliyokuwa imehifadhiwa au hata kuitengeneza toka tishu za mwili wenyewe ‘(gluconeogenesis)’.

Imethibitika pia kuwa kafeina imekuwa ikiingilia na kuathiri unakilishaji wa kinasaba (DNA), namna ambavyo seli mpya hutengenezwa. Kafeina inaweza kusababisha upotevu toka mwilini wa vitamini nyingi za kundi B, kundi C, zinki, potasiamu na madini mengine. Kahawa huongeza hali ya uasidi kwenye utumbo mdogo.

Kafeina inaweza kusababisha msukosuko ndani ya mwili.
Kafeina siyo kwamba tu huimaliza nguvu iliyokuwa imehifadhiwa kwenye ubongo, bali pia huzuia mfumo vimeng’enya katika kutengeneza kumbukumbu kwenye ubongo.

Kituo cha Sayansi kwa maslahi ya umma (Center for Science in Public Interest) kimewashauri kinamama wajawazito kukaa mbali na kafeina kwa kuwa tafiti zimeonesha kwamba kiasi cha kafeina kilichomo kwenye vikombe 4 vya kahawa kwa siku kinaweza kusababisha matatizo wakati wa kujifungua kama yalivyoonwa katika majaribio kwa wanyama.

‘Madawa na wewe’, kwa mjibu wa Dr. Earl Mindell, mwandishi wa kitabu; ‘Earl Mindell’s New Vitamin Bible’ (zaidi ya nakala milioni 10 zimeuzwa), anasema katika ukurasa wa 414 wa kitabu hicho kuwa ‘kafeina ni dawa yenye nguvu kubwa, uwezekano ni kuwa, hauifurahii tu kahawa au cola yako ya kila siku, bali umekuwa mtegemezi au teja (addicted) wa hiyo kafeina’.

Madhara ya chai ya rangi na kahawa mwilini ni mengi sana na tatizo moja litapelekea lingine na orodha inakuwa haiishi.

Namna ya kuepuka kaffeina kwenye kahawa na chai:
Badala ya kutumia majani hayo ya chai meusi, wewe chemsha maji yako ya chai kama kawaida na unaweza kutumia vifuatavyo kukamilisha chai yako; unaweza kutumia tangawizi na kumbuka pia tangawizi ni dawa ya zaidi ya magonjwa 72 mwilini.

Kwahiyo unapoinywa chai ya tangawizi siyo tu unaepuka madhara ya kaffeina peke yake, bali pia unakuwa umekunywa dawa ya zaidi ya magonjwa 72 mwilini!. Unaweza pia kuweka mdalasini, mchaichai, kukamulia ndimu, pia unaweza kutumia mchanganyiko wa viungo vingi vya chai (spiced tea) ambavyo vinapatikana kwa wingi katika soko la Kariakoo Dar – Es – Salaam na Zanzibar.

MAYAI YASIPOIVA NI HATARI

Mayai ni moja ya vyakula vyenye viini lishe muhimu kwa ajili ya afya ya mwili wa binadamu. Kwa kawaida mayai kabla ya kuliwa, huandaliwa kwa njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuchemshwa, kukaangwa au kuchanganywa na vyakula vingine kama vipande vya viazi mviringo ambavyo ni maarufu kwa jina la chips.

Pia, kuna baadhi ya watu wanaopendelea kula mayai mabichi kama dawa ya tiba mbadala, kwa ajili ya kulainisha sauti na wengine hupendelea kula mayai ya kukaanga ambayo hayakukaushwa vizuri.
Ukitembelea migahawa mingi utabaini kuwa watu wanakuwa na mitazamo tofauti na wanavyopenda kula mayai.

Mfano kuna wanaoagiza watengenezewe mayai kwa mtindo unaojulikana kama ‘macho ya ng’ombe.’ Ukiagiza namna hiyo, mpishi atataka kuuliza kama ni ‘macho ya ng’ombe’ ya kugeuza.

Ina maana kuwa ‘macho ya ngombe’ ya kugeuzwa ni yale yanayoivishwa pande zote lakini yale ambayo siyo ya kugeuza, huwa linaiva nusu. Upande mmoja unabaki ukiwa mbichi, na ndiyo raha ya baadhi ya watu.

Hata ukienda kwa wakaanga chipsi, utakuta wanawauliza wateja wao kama wanapokaanga na mayai wakaushe au wasikaushe. Hii inaashiria kuna watu wanataka wale chipsi zikiwa na mayai ambayo halijaiva sawasawa.

Kuna watu wengine wanaamini kwamba kula mayai mabichi kunafanya sauti inakuwa nyororo, hivyo wale waimbaji huwalazimu kufanya hivyo ili kufanya nyimbo zao zivutie.

Si hivyo tu, kuna baadhi ya watu huamini pia dawa ya kikohozi ni kunywa yai bichi lililochanganywa na asali. Hizi ni imani ambazo zimejengeka kwenye jamii na watu hufanya hivyo ili kufikia malengo waliyokusudia.

Katika siku za karibuni, imevuma kuwa mayai ya kwale yanatibu magonjwa sugu kama vile kisukari, shinikizo la damu, saratani na kifua.

Katika mpango huo, wanapendekeza wahusika kula mayai mabichi ya kwale tena kwa kutafuna hadi kaka lake, yaani ganda la nje.

Hali hii imesababisha biashara ya mayai ya kwale kuwa kubwa na hata wafugaji wameongezeka mara dufu.

Thursday, May 11, 2017

Zifahamu faida juisi ya nanasi mwilini mwako

Nanasi ni moja ya tunda ambalo hupendwa na watu wengi ulimwenguni si kwasababu ya  kutokana na kuwa na ladha nzuri pia.

Matumizi ya juisi halisi ya nanasi huenda yakawa na faida pia katika miili yatu kutokana na kuwa na virutubisho kadhaa ambavyo ni muhimu mwilini pia.

Miongoni mwa faida za kunywa juisi halisi ya nanasi ni pamoja na;

1. kusaidia mmen’genyo wa chakula kuwa katika hali nzuri zaidi.
2. Kunywa juisi ya nanasi pia huasidia sana kuimarisha mifupa ya mwili, kutokana na juisi hiyo kuwa na madini ya ‘manganese’. Kimsingi glasi moja ya juisi ya nanasi ni sawa na kupata asilimia 73 ya madini hayo ya manganese. Hivyo nanasi husaidia ukuaji wa mifupa kwa watoto wadogo pamoja na kuimarisha mifupa wakati wa umri mkubwa (uzeeni).

3. Pia unywaji wa juisi ya nanasi husaidia sana kuongeza kinga ya mwili pamoja na kuboresha afya ya ngozi, huku ikisaidia pia katika kumpatia mhusika uwezo mzuri wa kuona na hii ni kutokana na kuwa na vitamin A ndaini yake. Hivyo matumizi ya mara kwa mara ya juisi ya nanasi yataweza kukusaidia kuepuka matatizo ya kuwa na uoni hafifu hapo baadaye katika umri mkubwa.

4. Hutibu maumivu ya viungo.
Kunywa juisi hii ya nanasi pia kutasaidia sana kukuondolea tatizo la kuhusi maumivu ya viungo ‘arthritis’. Juisi ya nanasi husaidia sana kupunguza maumivu ya viungo kwa watu wazima (wazee) ambao mara nyingi wamekuwa wakisumbuliwa na matatizo hayo.

5. Hutibu matatizo ya kukosa choo.
Ukweli ni kwamba juisi ya nanasi imebarikiwa kwa kusheheni madini na vitamin nyingi za kutosha sana. Kuhusu vitamin juisi hii ina vitamin C, B Complex, na imebarikiwa pia kuwa na madini ya 'potassium', 'calcium', 'manganese' na 'phosphorous', huku ikiwa na utajiri mkubwa wa 'fiber' yaanu nyuzinyuzi ambazo huwa na umuhimu pia na kukinga dhidi ya tatizo la kukosa choo ‘consumption.’

6. Ni hongeza kinga dhidi ya magonjwa mbalimbali.
Juisi halisi kabisa ya nanasi huwa na asilimia 75 ya kiwango cha vitamin C , huku vitamin hiyo ikiwa ni muhimu sana katika mfumo wa kinga mwilini.

Nanasi pia linauwezo wa kukuepusha na matatizo ya shinikizo la damu yaani high blood pressure, kwahiyo inashauriwa mtu mwenye tatizo hilo kujenga utamaduni wa kutumia juisi ya nanasi mara kwa mara.

7. Hulinda afya ya meno.
Kimsingi kuna mengi ya kuzungumza kuhusu faida za juisi hii, lakini kwa ufupi ni kwamba faida nyingine za juisi hii ni kulinda afya ya meno na moyo pamoja na kuwasaidia wale wenye kuhitaji kupunguza uzito.

Magonjwa yanayotibika kwa Mmea Mnyonyo


Magonjwa yanayotibika kwa mmea mnyonyo
  • mnyonyo una faida nyingi
  • sana  kwa afya ya mwanadamu.
  • Karibu kila kitu  kinachopatikana
  • kwenye mmea wa  mnyonyo  kina
  • faida za kiafya kwa mwanadamu.


Magonjwa yanayotibikwa kwa mnyonyo.

  1. Kwikwi :Jaza maji kwenye kikombe, mpe mgonjwa anywe kila baada ya dakika 3 mpaka kwikwi iishe.
  2. Kuungua :Meza punje za mti wa
  3. nyonyo kwa maji kiasicha glasi moja kwa siku kwa muda wa siku
  4. tano.
  5. Kutibu miguu inayouma.
  6. Tumia majani kwa kufungia miguu inayouma.
  7. Maumivu Ya Mgongo.
  8. Majani yake ukiyapasha moto yafaa kukanda mgongo wenye
  9. maumivu.
  10. Kutibu Kaswende na Kisonono.


Unachotakiwa kufanya;
Ponda mizizi ya mti wa mnyonyo, kisha  chemsha na tumia kunywa glasi moja mara mbili kwa siku kwa muda wa siku saba.

Kusafisha utumbo: Kunywa mafuta ya mnyonyo vijiko viwili vikubwa vya chakula asubuhi, kisha pumzika kwa saa mbili ndipo unywe maji glasi mbili na endelea kunywa maji glasi moja kila baada ya saa moja.

Mnyonyo unaweza pia kuwafaa watu wanaoishi na VVU (Virusi Vya UKIMWI) kwani mafuta yake ni sumu ya kuua vimelea vya magonjwa kama vile bakteria na ukungu (fungus).

Namna ya kufanya:
1. Kupakaza: Chukua kipande cha nguo ama kitambaa, kisha kiloweke kwenye mafuta ya mnyonyo ndipo ufunge katika kiwiko ama eneo lenye maumivu ama kidonda. Vinginevyo, chukua kiasi cha mafuta na kupaka eneo linalohusika mfano, penye kidonda, kuugua ama pakaza kichwani au juu ya tumbo wakati wa maumivu ya hedhi nk. Unaweza kuacha kwa muda wa saa moja kabla ya kunawa ili uipe ngozi muda wa kunyonya kiasi cha mafuta. Unaweza kujifunga kitambaa hicho tumboni ama mgongoni kama kibwebwe na kuendelea na shughuli za kawaida.

2. Kunywa: Chemsha mbegu chache za mnyonyo pamoja na maji na maziwa kisha unywe kiasi kidogo kadiri ya nusu hadi bilauri moja ya ujazo wa mili lita mia mbili na arobaini.