Kwikwi hutokana na kushtuka na kusinyaa kwa ghafla kwa misuli mikuu ya upumuaji (diaphragm) ambako hujirudia rudia na kusababisha hewa kuingia kwa kasi kwenye mapafu.
Hii husababisha milango ya sauti katika koo (vocal cords or voice making cords) kufunga ghafla na kutoa sauti inayosikika wakati wa kwikwi.
Kwikwi sio ugonjwa; kwikwi ya muda mfupi ni kero ndogo tu ambayo inapita, lakini kwikwi isiyokatika inaweza kuwa dalili ya tatizo lingine ambalo huenda likahitaji uchunguzi wa kitaalamu.
Sababu zinazopelekea kupata kwikwi;
- Kula haraka haraka au kula sana (kuvimbiwa)
- Kula vyakula vyenye viungo sana (very spicy foods)
- Kunywa vinywaji vyenye gesi(carbonated beverages) au vya baridi sana
- Ulevi au kunywa pombe nyingi kwa mpigo
- Upungufu wa maji na madini mwilini (dehydration)
- Tumbo kujaa gesi, asidi (hyperacidity) au vidonda vya tumbo
Sababu hizi mara nyingi husababisha kwikwi ya muda mfupi ambayo huisha bila kuhitaji matibabu wala uchunguzi wa kitaalamu.
Sababu nyingine (Rare but serious) ni pamoja na;
- Upungufu au kuvurigikwa kwa kiasi cha madini mwilini(electrolyte imbalances)
- Kukusanyika kwa sumu mwilini kama vile sumu ya figo (Uremia)
- Magonjwa ya mapafu kama vile vichomi(pneumonia), pumu(asthma), TB au maji kukusanyika nje ya mapafu(pleural effusion),
- Saratani au uvimbe kwenye mapafu, ubongo, uti wa mgongo au tumboni.
- Magonjwa ya moyo (heart attack, arrhythmias, infections to the heart)
- Kidole tumbo(Apendix illness) na magonjwa ya kufanania nayo
- Magonjwa ya Ini, kongosho au mfuko wa nyongo
- Madawa au kunywa sumu aina fulani
- Kuumia katika eneo la misuli ya upumuaji (diaphragm injuries).
Kwikwi itokanayo na matatizo haya huwa ya muda mrefu au inayojirudia rudia sana, na huisha tu kama tatizo lililosababisha likigundulika na kutibiwa. Ukiona dalili ya kwikwi isiyoisha tafadhali muone daktari.
Sababu ya kisaikologia (psychological reason)– Hii huwapata watu wachache. Watu hawa hujidhania kuwa wana kwikwi isiyokatika, hivyo huendelea kutoa sauti kama mtu mwenye kwikwi. Kwikwi ya aina hii haina mfumo maalum, na haitokani na kusinyaa kwa misuli ya upumuaji; kwa mtu mwenye tatizo hili ni muhimu kutafuta tatizo alilo nalo kisaikologia na kulitatua.
Namna ya Kuzuia Kwikwi
- Kula taratibu – haraka haraka hujaza gesi tumboni na kusababisha kuvimbiwa
- Kula kiasi kidogo kwa wakati – Inashauriwa kuongeza idadi ya milo kwa siku badala ya kiasi; milo mitano midogo midogo badala ya mitatu mikubwa kwa siku.
- Punguza au ondoa kabisa vyakula vyenye viungo vingi/vikali.
- Kunywa maji – Unywaji mzuri wa maji huzuia na kutibu kwikwi, pia hulinda mwili na maradhi kama vile upungufu wa maji na madini(dehydration) na figo kutofanya kazi vizuri.
- Fanya mazoezi - huboresha ufanyaji kazi wa mapafu na misuli ya upumuaji, pia husaidia kuongeza kinga mwilini na kuimarisha ufahamu (mind state)
Kuzuia kwikwi ni muhimu tu kwa wale wanaopata mara kwa mara.
Matibabu ya kienyeji: (Usifanye kwa mtoto)
- Kumshitua mhusika, au kumzubaisha ili kuondoa mawazo yake kwenye kwikwi
- Kunywa glasi ya maji iliyojaa bila kukata pumzi
- Kubana pumzi na kuhesabu mpaka kumi
- Kuweka sukari chini ya ulimi
- Kulala. Usingizi ni dawa moja nzuri sana ya kwikwi
- Kwa mtoto anayenyonya waweza kumnyonyesha, au kumuweka begani acheue.
- KWIKWI-twanga hiliki changanya na maziwa kisha kunywa glasi moja.
Matibabu ya kitaalam
Muone daktari kwa matibabu kama
- Kwikwi haikatiki kwa muda mrefu (siku au zaidi),
- Kwikwi inakusababisha kuchoka sana,
- Kama mapigo ya moyo yanabadilika,
- Kama unashindwa kulala kutokana na kwikwi
- Kama inasababisha msongo mawazo kutokana na kujirudia mara kwa mara.
Kabla ya kuanzisha dawa ni muhimu kufanya vipimo ili kuhakikisha magonjwa yanayoweza kusababisha kwikwi yanapatiwa matibabu kama yapo.
Kama chanzo cha kwikwi kimefahamika katika uchunguzi, tibu chanzo na kwikwi itaisha.
Asante na nimeelew
ReplyDeleteOk,thanks Sana.Nimekuelewa sana
ReplyDeleteNashkr kwa mafundisho hayo ya kwikwi,but mimi inansumbuaga sana na waga mimi inanirudia Mara kwa mara
ReplyDeleteRafiki naomba unitafut mana mm pia nina tatiz kama la kwako.
DeleteHedimeninocenti@gmail.com
O623221279
Thnx Dear, nimepata Mwanga kidogo
ReplyDeleteAsante sana
ReplyDeleteAsante kwikwi inaboa leo siku ya tatu inaacha nikiogopa tu nje ya hapo njia nyingine hazinisaidii na kwa kweli naumia sana kifuani
ReplyDeleteTatizo lako kama langu dear
DeleteDaah kwikwi inaboa mno,,bora mwanga umeptkn kdg
DeleteNenda hospitali
ReplyDeleteAsante kwa ushauri wenu
ReplyDeleteOoh nimejifunza mengi kupitia makara yako may God bless you
ReplyDeleteAsanteni kwa ushauri wenu
ReplyDeleteAthumanimdee66@gmail.com
ReplyDeleteAsante kwa ushauri maana huwa inanitesa sana tena wakati wa usiku nikilala nikishuta usingizini BC kwikwi ndio anashika hadi mchana
ReplyDeleteAsante sana kwa elimu
ReplyDeleteTHANKS FOR GOOD PICTURE
ReplyDeleteThanks for what you teach us
ReplyDeleteAsante imenitesa siku mbili hizi
ReplyDeleteNice
ReplyDeleteNice
ReplyDeleteNashukuru sana kwa maelezo yako maana inanisumbua sana kwikwi
ReplyDeleteJee kwiki inawez kuuwa ina nisumbua sana mpka naogopa natumia sana maji
ReplyDeleteAhsante kwa somo
ReplyDeleteDeal done good job stay blessed our supervisor
ReplyDeleteAhsante sana kwa maaelezo na ufafanuzi mzuri juu ya kwikwi, Endeleeni kutoa Elimu ya afya ilimtuendelee kuwa na taifa lenye watu wenye afya njema!
ReplyDeleteMtoto wangu ana kwikwi tokea mchanga hafi leo ana miaka miwili, ila inamjia endapo tu ataanza kucheka huja gafla mda huohuo , je husababishwa na nini haswa??!
ReplyDeleteNice one
ReplyDeleteSafi.ubarikiwe
ReplyDeleteThanks good matter
ReplyDeleteAsante sana
ReplyDeletesawa nimeelewa
ReplyDeleteBaba yangu anasumbuliwa na kwikwi Sana nipo nae hospital wamempa dawa ila naona Bado.... Namwamsha Nampa maji inakata kidogo inarudi Tena ...sijui nifanyaje maana Leo siku ya pili hata haimpi kulala
ReplyDelete