Sunday, July 30, 2017

Athari za kiafya za vyakula vyenye Wanga

MOJA ya vyakula ambavyo tumekuwa tukitumia kwa wingi hasa Watanzania wenye kipato cha kati na chini kabisa ni vyakula vya aina kuu tatu, Wanga, Protini na Mafuta (Fats).

Na kwa kiwango kidogo sana tunatumia vitamin na madini katika milo yetu. Moja ya masomo ya chakula tunayofundishwa ni kula mlo kamili.Watu wengi tumekuwa tukitumia elimu hiyo hadi hapa tulipofika.

Napenda kusema tu kwamba mlo kamili ni kwa ajili ya mtu mzima ambaye hana ugonjwa wowote na ni kwa yule tu ambaye hataki kula kiafya.

Napenda kusema haya kwa sababu tumekuwa tukila vyakula vya namna ile ile lakini tumekuwa tukiugua mno magonjwa mbalimbali yatokanayo na lishe mbovu. Hadi sasa ugonjwa wa kisukari hapa duniani unaua zaidi ya ugonjwa wa UKIMWI, swali la kujiuliza je, tumejitenga wapi mbali katika lishe?

Leo nataka nikueleze kidogo kuhusu sayansi ya chakula aina ya wanga. Maana kila mtu ninayemwelekeza njia sahihi ya kupunguza uzito anakwambia nitaishije bila chakula cha wanga? Mwili wako hutumia vyakula vikuu aina tatu ambavyo ni wanga, protini na mafuta.

Na unatakiwa ujue kuwa gramu moja ya wanga hutengeneza nishati ya mwili kalori nne, ambapo protini nayo hutengeneza kalori nne na Fats hutengeneza kalori tisa. Unaona ni zaidi ya mara mbili ya nishati zinazotengenezwa na chakula cha wanga.

Hii ina maana kuwa ninaposema kuwa tunaweza kupunguza wanga na ukaishi ukiwa na nguvu nyingi zaidi hata ya ulivyo kuwa katika lishe ya wanga nyingi.

KWA NINI NAKUSHAURI UPUNGUZE WANGA KIAFYA?
Unapokuwa umepunguza wanga au kuacha kabisa ulaji wa vyakula vyenye wanga nyingi, mfano mikate, ugali, wali na tambi. Hakikisha kitendo hicho kiendane na kuongeza kiwango cha mafuta na vyakula vya protini mwilini mwako katika lishe yako. Hii itaufanya mwili wako kuanza kutumia mafuta kama nishati ya mwili ya kwanza kujitengenezea nguvu.

Viungo vya binadamu kama ini na figo vinapokuwa vinatumia mafuta kuzalisha nishati ya mwili hutengeneza viini vya nishati viitwavyo Ketone Bodies, ambavyo hivi ndivyo hutumiwa na seli za mwili kujitengenezea nishati kwa wingi.

Hivyo basi, unapokuwa unajizuia kutumia vyakula vya wanga mwili wako utatumia karibia siku tano hadi wiki kuanza kutumia mafuta kama nishati ya mwili na hicho kitendo tunaita Keto Adaption.

Ningependa kusema kwamba Keto Adaption ni ile hali ya mwili wako kujenga mazoea ya kutumia mafuta kama chanzo cha nishati ya mwili na hapo ndipo utaanza kuona mabadiliko katika mwili wako makubwa.

Utakuwa unajisikia mwenye nguvu na unatashangaaa dalili mbalimbali zilizokuwa zinakusumbua zinapotea hii ni kwa sababu ya uwezo mkubwa wa ketone bodies katika mwili wako dhidi ya glucose.

Sote tunajua kwamba ulaji wa vyakula vya wanga kwa wingi na vyakula vyenye sukari nyingi vinaongeza kiwango cha sukari kwenye damu zaidi ya kiwango ambacho mwili wako unaweza kuhimili.

Mfano; kiwango cha kawaida cha sukari kinachohitajika mwilini mwako ni kijiko kimoja cha chai, hiki ni kiwango ambacho hakiwezi kukuletea matatizo. Basi kama binadamu anaishi kwa sukari inayokadiriwa kuwapo kwenye damu kama kijiko kimoja tu cha chai.

Unywaji wa soda moja unaweza kuongeza zaidi ya vijiko 10, hivyo basi mwili wako unakuwa unashindwa kuhimili sukari iliyozidi.

Kwa wale wanaopenda kula baga, inakadiliwa kuwa baga moja ya kati inaweza kutoa sukari zaidi ya vijiko 16 kwenye damu.

Swali la kujiuliza mwili unapeleka wapi sukari iliyozidi wakati miili yetu inahitaji sukari kiwango kidogo kama kijiko kimoja tu kuishi?
Mwili hutengeneza maji kutoka kwenye seli za kongosho ziitwazo beta seli, maji haya ni homon iitwayo Insulin, kazi kubwa ya insulin ni kutunza glucose hii katika damu kwa matumizi ya baadae, na inatunza katika kiasi maalumu katika mfumo wa Glycogen na kiasi kikubwa katika mafuta.

Hivyo basi, mafuta haya huhifadhiwa katika sehemu mbalimbali kama tumboni, shingoni, mikononi, kifuani na kiunoni. Mafuta haya huhifadhiwa katika mfumo wa Tryglycerides ambayo haya ni miongoni ya mafuta mabaya mwilini mwako.

Sasa mtu anayekwambia wanga nyingi katika chakula chako ni salama anakudanganya kwa kiasi kikubwa kwani tunaona jinsi gani ulaji wa kiwango kingi cha vyakula vya wanga na sukari vinavyosababisha sukari kupanda kupita kiasi na insulin kuanza kuhifadhi katika mafuta.

Kila siku nasema, tumekaririshwa adui mkuu ni fats na kujisahau ulaji mbovu wa vyakula vya wanga huku tukiishia kulea vitambi na magonjwa sugu, hii yote ni kutokuwa na ufuatiliaji wa lishe nzuri na salama kwako.

MADHARA MENGINE YA SUKARI
Napenda kuwarudisha nyuma kidogo katika somo la bailojia. Tulijifunza kuwa miili yetu imejengwa kwa kiini kidogo sana kiitwacho seli ambapo shughuli zote za mwili zinafanyika humo.

Nilijifunza kuwa ndani ya seli kuna viungo vidogo vidogo navifananisha na (Apartments kwenye nyumba kubwa) moja wapo ni Mitochondria, hiki ni kiungo kidogo katika seli ambacho kinahusika na kuzalisha nishati ya mwili tu. Pia nikikumbuka watu wote tulijifunza kwamba mwili wetu hujitenegenezea nishati ya mwili au nguvu kupitia kuifanyia kazi sukari iliyo ndani ya damu baada ya kuingia ndani ya seli.

Hivyo basi insulin ni kama ufunguo ambao unafungua milango ili sukari iweze kuingia ndani ya seli hadi kwenye mitochondria. Mwili wako unapokuwa unatumia hewa ya oxygen kuna uwezekano mkubwa wa kupatikana kwa athari iitwayo Oxdative stress.

Hii ndiyo inayofanya chuma kipate kutu, hii ndiyo inayofanya mafuta ukiyaweka kwenye jua kwa muda mrefu yanaharibika. Basi mwili wako unakuwa unatengeneza vihatarishi viitwavyo Reactive Oxygen Species kwa kifupi huitwa Free Radicals.

Hizi ni sumu ambazo hupatikana wakati mwili unajitenegenezea nishati yake kwa kutumia oxygen na hizi zinapokuwa kiwango kikubwa huweza kuharibu kabisa seli na kuziua na pia zinaweza kupelekea kupata magonjwa sugu kama saratani.

Hivyo, tafiti zinaonesha kwamba vyakula vya wanga na sukari vina matokeo makubwa ya kutenegeneza Free Radicals nyingi kupita kiasi.

Miili yetu ina kiwango fulani cha viondoa sumu ambavyo vinaipunguza sumu ya free radicals kuepusha kusababisha magonjwa kwa kuziua seli.

Lakini panapokuwa na kiwango kikubwa cha uzalishaji wa free radicals mwili unashindwa kuhimili na hatimaye free radicals zinaanza kuleta madhara mwilini mwako. Kadri mitochondria zinavyodhoofika ndivyo magonjwa nyemelezi ya lishe yanavyotukabili kila kukicha.

Monday, May 29, 2017

Je unayo mawe kwenye figo? soma hapa

UGONJWA wa mawe kwenye figo siyo mgeni miongoni mwa watu hivi sasa, hasa wenye umri mkubwa. Hata hivyo, katika siku za hivi karibuni, ukubwa wa tatizo hili umeongezeka, kwani hata vijana wanapatwa na tatizo hili ambalo kitalaamu linajulikana kama ‘Gallstones’.

Mawe ya kwenye figo siyo mawe halisi, bali huwa ni vitu vinavyojitengeneza kwenye figo taratibu na baada ya muda mrefu hugeuka umbo na kuwa mfano wa vijiwe vidogo na wakati mwingine huwa vikubwa mfano wa dole gumba. Hutokana na ulaji wa vyakula usio sahihi.

Tiba ya tatizo la mawe kwenye figo, mara nyingi huwa ni upasuaji wa kuvitoa na hugharimu fedha nyingi na pia husababisha maumivu wakati wa kufanya oparesheni hiyo. Lakini kwa kutumia tiba mbadala ya vyakula, unaweza kuondoa mawe hayo bila kufanya oparesheni.

Maelezo haya huwezi kuambiwa na daktari hospitali hata siku moja lakini kwa kusoma makala kama haya utajifunza njia nyingine ya kuutibu mwili wako kwa njia ya vyakula. Kama mawe yaliingia tumboni kwa njia ya vyakula, bila shaka yanaweza kutoka pia kwa vyakula.

JINSI YA KUONDOA MAWE KWENYE FIGO
Kuna tiba mbadala za aina nyingi, lakini katika makala yangu ya leo nitawajulisha njia mbili unazoweza kuchagua moja wapo. Moja ni kufanya kwa muda wa siku sita mfululizo na nyingine ni ya kufanya kwa siku moja tu, chaguo ni lako.

NJIA YA SIKU SITA
Katika siku tano za kwanza, kunywa juisi halisi ya Tufaha(pure apple juice) glasi kubwa nne kila siku kwa siku tano mfululizo. Au kula tufaha nzuri tano badala ya juisi. Ili kuwa na uhakika na juisi halisi, ni vyema ukanunua tufaha za kijani (green apple) na ukatengeneza juisi mwenywe. Juisi hii au matufaha hayo yatafanya kazi ya kulainisha kwanza mawe tumboni.

Siku ya sita, anza siku yako kwa kula mlo wako wa kawaida hadi saa nane mchana, kuanzia saa nane utatakiwa ufunge usile kitu chochote mpaka asubuhi siku inayofuata ndiyo ule chakula chako.

Ifikapo saa 12 jioni, kunywa kikombe au glasi moja kubwa ya maji uliyochanganya na kijiko kimoja kidogo cha ‘Magnesium Sulphate’ . Weka maji kwenye glasi au kikombe, chukua ‘Magnesium Sulphate’, chota kijiko kimoja kidogo, tia kwenye maji hayo na changanya, kisha unywe mara moja. ‘Magnesium’ husaidia kufungua njia.

Ifikapo saa mbili usiku, rudia kunywa mchanganyiko huo wa maji na ‘Magnesium’. Baadaye saa 4 usiku, changanya nusu kikombe cha juisi halisi ya limau (fresh lemon juice) na nusu kikombe cha mafuta halisi ya mzaituni (pure olive Oil). Hiki ndiyo kitakuwa kinywaji chako cha mwisho kwa usiku huo, kisha nenda kalale.

Vinywaji hivyo vitasaidia mawe kutoka kwa njia ya haja kubwa bila shida. Usiku huo huo, unaweza kusikia haja ya kwenda chooni, au vinginevyo utasikia asubuhi.

NJIA YA SIKU MOJA
Ukisha kula chakula chako cha usiku, usile kitu kingine tena hadi kesho yake asubuhi ambapo utakunywa glasi kubwa tatu za juisi ya tufaha za kijani. Usile kitu kingine hadi mchana unywe tena juisi ya tufaha 3. Usile kitu kingine tena hadi usiku wakati wa chakula cha usiku, unywe tena juisi ya tufaha kubwa 3 za kijani kama mlo wako wa usiku.

Iwapo utashindwa kutengeneza juisi mwenywe, basi bora ule tufaha zenyewe kiasi kilichotajwa. Katikati ya mlo na mlo, utaruhusiwa kunywa maji ya kawaida tu na siyo kitu kingine. Hii ina maana utafunga siku moja kwa kula tufaha na maji tu.

Muda mfupi kabla ya kwenda kitandani, tengeneza juisi halisi ya malimau matatu, changanya na nusu kikombe cha mafuta ya mzaituni (Pure olive oil) kunywa kisha panda kitandani, kinywaji kinaweza kisiwe na ladha nzuri, lakini usijali, ndiyo dawa.

Ukiwa kitandani, lalia ubavu wako wa kulia na ukunje magoti kadiri uwezavyo na ulale hivyo kwa muda utakaoweza au hadi hapo utakapopitiwa na usingizi. Ulalaji wa aina hii huwezesha utokaji wa mawe kwenye figo na kwenda tumboni kwa ajili ya kutoka kwa njia ya haja kubwa.

Ukijisikia haja ya kwenda chooni, fanya hivyo haraka, vinginevyo utalala hadi asubuhi ndiyo utakwenda chooni. Ili kuona kama vimawe vimetoka, weka utaratibu wa kukagua haja yako na utaona vitu rangi ya kijivu au kijani vinavyong’aa na hapo utakuwa umefanikiwa.

Mbinu za Kutunza Ngozi yenye Mafuta

Sababu ya ngozi kuwa na mafuta hutokana na  na tezi za sebaceous na kuzalisha mafuta zaidi ya kiwango ambacho ambacho kinatakiwa. Lakini licha ya tezi hizo aina za sebaceous kuzalisha kiwango cha mafuta kwa wingi, zipo pia sababu nyingine ambazo zinafanya ngozi kuwa na mafuta ambazo kama ifuatavyo.

    1. • Kurithi.
    2. • Lishe.
    3. • Kiwango cha homoni mbalimbali mwilini.
    4. • Ujauzito.
    5. • Baadhi ya vipodozi .
    6. • mabadiliko ya hali ya hewa hasa joto.

              Na madhara ambayo yanatokana na ngozi yenye mafuta ni kwamba, ngozi huweza kutengeneza ngozi yenye tabaka lisiloisha vipele pamoja na  chunusi kwa muda mrefu.

              Baada ya kuona baadhi ya sababu na athari ya ngozi kuwa mafuta,  sasa tuangalie namna ya kutunza ngozi zenye mafuta:

              1. Ngozi yenye mafuta inahitajia kusafishwa vyema kwa maji ya moto na sabuni ili kuzuia vinyweleo visizibwe na mafuta. Lakini Jitahidi kuitunza vyema ngozi yako na kuisafisha vizuri. Jaribu kuosha uso mara mbili au mara tatu kwa siku. Usioshe mara nyingi kwani kufanya hivyo huufanya uso kutoa mafuta zaidi.

              3. Epuka kutumia vipodozi ambavyo huifanya ngozi yako ipoteze maji au kukauka. Kwani husababisha sehemu ya juu ya ngozi inyauke, na hivyo kusababisha mafuta kuziba vinyweleo na kupelekea kutokea kwa chunusi ambazo zitaufanya mwili kuwa na mafuta.

              4. Chagua kile unachosafishia kwa makini, jiepushe kutumia cream nzito nzito au vifaa vugumu wakati wa kuosha uso wako. Ni bora utumie sabuni za kawaida zisizokuwa na madawa. Unaweza kutumia lotion ya kuua bacteria au sabuni zisizo na dawa nyingi (lightly medicated), au sabuni zenye madini mbalimbali. Ni bora usioshe au kutumia lotion au michanganyiko yenye alkoholi.

              5. Lakini pia unashauriwa ya kwamba hakikisha unatumia  mafuta ambayo  yametengenezwa kwa ajili ya ngozi yenye mafuta.

              Endapo utayazingatia hayo mwili wako utakwenda kuwa katika hali ya ubora zaidi, na kufurahia ngozi isiyo na kasoro. 

              Sunday, May 28, 2017

              Maumivu Wakati Wa Kufanya Mapenzi Kwa Wanawake

              Maumivu wakati wa kufanya mapenzi ni hali inayojitokeza hasa kwa wanawake. Hujulikana kwa kitaalamu kama.

              dyspareunia. Maumivu haya yanaweza kutokea wakati wa kufanya mapenzi au baada ya kufanya mapenzi. Sababu kuu za maumivu haya mara nyingi ni magonjwa ya zinaa na kupungua kwa majimaji ukeni wakati wa ngono.

              Maumivu Wakati Wa Kufanya Mapenzi
              Unaweza kuwa unapata maumivu wakati tendo la ngono linaendelea. Mara nyingi maumivu haya huwa kwenye kuta za uke, shingo ya uzazi au chini ya kitovu. Sababu za maumivu haya ni;

              1. Kuchubuka ukeni kutokana na maji ya uke kupungua. Inawezekana kutokana na kutoandaliwa vizuri wakati wa mapenzi au uke kutotoa majimaji ya kutosha.
              2. Magonjwa ya zinaa kama kisonono, klamidia, vaginitis.
              3. Maambukizi ya shingo ya uzazi (cervicitis)
              4. Maambukizi kwenye mirija ya uzazi. Mara nyingi amumivu hutokea chini ya kitovu au kiuononi.
              5. Maumivu Baada ya Kufanya Mapenzi

              Baada ya kukutana na mwenzi wako kingono, unaweza kuanza kupata maumivu dakika chache mpaka siku kadhaa toka mlipokutana. Maumivu ya kawaida huwa ni kwenye uke kutokana na kuchubuka wakati wa kufanya mapenzi. Unaweza kuyahisi vizuri hasa pale unapojisafisha kwa maji au wakati wa kukojoa ikiwa njia ya mkojo imechubuliwa.

              Maumivu ndani ya uke kabisa, kiunoni au chini ya kitovu baada ya kufanya mapenzi mara nyingi huonesha dalili za

              • Maambukizi ya shingo ya uzazi
              • Maambukizi ya mirija ya uzazi
              • Saratani ya shingo ya kizazi

              Dalili hii inaweza kuambatana na hali ya homa, kutokwa damu ukeni baada ya ngono, kutoa uchafu ukeni, kutapika na kichefuchefu.

              Matibabu

              Unapopata hali hii jichunguze vizuri. Kama maumivu hayajatokana na michubuko wakati wa mapenzi, basi onana na daktari haraka iwezekanavyo. Maambukizi ya shingo ya uzazi na mirija ya uzazi (Pelvic Inflammatory Disease – PID) huchangia kwa kiasi kikubwa hali hii. Matibabu ya haraka ni muhimu ili kupunguza madhara ya magonjwa haya.

              Michubuko kutokana na kufanya mapenzi hupona yenyewe polepole. Jioshe vizuri kwa maji safi. Usipake dawa zozote mpaka uambiwe na daktari wako.

              Monday, May 22, 2017

              Tatizo la Kunuka Kikwapa, tiba hii hapa

              Kikwapa  ni  tatizo la kutoa harufu mbaya  sehemu ya kwapani katika mwili wa binadamu. Tatizo la kikwapa husababishwa na bakteria wanaovutiwa na jasho au unyevunyevu  chini ya kwapa.
              Tatizo la Kikwapa ni kero kwa sababu husababisha mtu kutoa harufu inayokuwa kero kwako na kwa mtu mwingine aliyeko jirani yako.

              Ili kwapa lako liwe na harufu nzuri, kavu na safi fanya yafuatayo
              • Paka kipande cha limao kwenye kwapa na kuacha lipate hewa  safi ili kuua vijidudu na kutoa tezi za jasho kuondoa harufu mbaya
              • Vaa nguo safi zenye nyuzinyuzi za asili kama pamba, hariri na sufu zitasaidia kufyonza unyevu na kuliacha kwapa lako kavu, safi na bila harufu mbaya
              • Oga kila siku na safisha nguo kwa maji safi itasaidia kuua bakteria na ambao husababisha harufu mbaya
              • Kunywa maji mengi kila siku yatakusaidia kutoa sumu mwilini na hivyo kupunguza harufu mbaya ya kwapa.
              • Osha kwapa mara kwa mara kwa kutumia sabuni zenye dawa (medicated soaps)
              • Punguza kula chakula chenye viungo vingi hasa vitunguu
              • Kumbuka kutumia pafyume na Spray zitasaidia kuondoa harufu mbaya kwa muda na sio kutibu tatizo moja kwa moja.
              • Baada ya kuoga jifute kwa taulo au kitambaa safi na usiache unyevu unyevu ambao uwavutia bakteria kukua katika eneo ili.
              • Jitahidi kunyoa nywele za sehemu hii mara kwa mara.
              • Epuka kukaa sehemu zenye joto kupita kiasi kwa muda mrefu.

              Magonjwa 10 ya kurithi ambayo ni muhimu kupima au kuyajua na mpenzi wako kabla ya kuzaa mtoto..

              Magonjwa ya kurithi ni yapi?
              Haya ni magonjwa ambayo yapo kwenye koo za watu fulani na hurithiwa kutoka kizazi mpaka kizazi lakini pia magonjwa haya huweza kutoka kwa mwanamke na mwanaume ambao kwa macho ni wazima kabisa na kuzaa watoto wenye matatizo ya kiafya.

              Kwenye jamii zetu za kiafrika ni jambo la kawaida sana kuzaa tu bila kupima kujua kama kuna hatari ya kuzaa mtoto mwenye matatizo makubwa ya kiafya kutokana na vimelea vya kurithi yaani DNA ambazo wazazi husika wamezibeba, mimba nyingi zimekua zikisingiziwa kwamba hazikupangwa na wakati kila mtu anajua mwisho wa ngono zembe bila njia yeyote ya uzazi wa mpango ni mimba.
              Hii ni tofauti na nchi zilizoendelea ambapo wazazi hupima vipimo hivi kabla ya kuamua kuzaa na hata ikigundulika mtoto anayekuja atakua na matatizo mimba hiyo hutolewa ili kuepusha maumivu ambayo mtoto huyo angeyapata kama angezaliwa na maumivu ya kisaikolojia na kiuchumi ambayo wazazi wanaozaa watoto kama hawa wanayapata, hii ni kwasababu ya kulazwa mara kwa mara kwa mtoto husika na kushindwa kufanya kazi maisha yake yote.

              Hivyo nchi zilizoendelea watoto wanaozaliwa na magonjwa ya kurithi wametokomezwa kwa kiwango kikubwa sana tofauti na afrika ambapo watoto hawa ni wengi sana na kila siku wanazidi kuzaliwa, wakati wangeweza kuzuilika kama sisi wahusika na serikali ingechukua hatua kukomesha hili kwa kuingiza vifaa vya kitaalamu ya kuyagundua magonjwa haya muhimu.
              Ni kweli vipimo vingi havipatikani hasa maeneo ya vijijini na hata mijini lakini kuna watu ambao wako kwenye nafasi kubwa ya kuzuia na kupunguza idadi ya watoto hawa wanazaliwa kila siku, hasa watu wanaoishi mijini na wenye uwezo kifedha lakini hata wewe ambaye huwezi kupata vipimo hivi hebu jaribu kwenda ukweni kwa mumeo au mkeo unaweza ukaona ugonjwa wa kurithi ambao sio wa kawaida huko na kufanya maamuzi vizuri au unaweza ukamuuliza mumeo au mkeo ili awe muwazi kabla ya kufunga ndoa kwani magonjwa mengine yanaonekana kwa macho tu.
              Magonjwa haya ni kama yafuatayo…

              1.Sickle cell disease;{siko seli] huu ni ugonjwa wa kurithi ambao mtoto hurithi kutoka kwa baba na mama ambapo wazazi wawili ambao wanakua hawana dalili yeyote hubeba ugonjwa huu kwenye damu zao yaani carrier na wanakua na uwezekano wa 25% ya kumzaa mtoto huyu ambae ataugua na kua na dalili zote za ugonjwa huu. Ugonjwa huu ni hatari sana. Mwaka 2013 ugonjwa huu uliua watu laki mmoja na elfu sabini na sita duniani kote wengi wakitokea Africa hasa chini ya jangwa la sahara. Watoto hawa huanza na dalili za kuvimba vidole wakiwa na umri wa miezi mitatu, kuvimba vichwa, kua na miguu na mikono mirefu na miembamba, kulalamika maumivu makali, kuishiwa damu sana  na kadhalika ukubwani. Kama wapenzi wakipimwa wakakutwa wote wameubeba ugonjwa huu kwenye damu zao yaani carriers ni vizuri wakaairisha ndoa hiyo kwani watakaribisha matatizo makubwa kwenye maisha yao. Kama unataka kujua umebeba ugonjwa huu ukienda hospitali kubwa za rufaa wana uwezo wa kuwapima na kujua. Ugonjwa huu pia unaweza kupimwa kwa kuchukua maji kwenye tumbo la mama kabla hajazaliwa hivyo kuamua kuendelea na mimba au kuitoa. Japokua kutoa ni kosa kisheria nchini Tanzania. Watoto hawa huishi kwa mateso makali na 50% watakufa kabla ya miaka 40 kwa nchini kwetu Tanzania hakuna data kamili za watu hawa lakini wasichana wengi wenye ugonjwa huu hufa wanapoanza kuziona siku zao kwani damu hupungua zaidi na viungo vingi kushindwa kazi.
              2.Haemolytic diseases of the new born;  kuna aina kuu nne za group za damu yaani A, B, AB, na O ambazo group hizo mtu anaweza kua positive au negative mfano mtu mwingine anaweza kua A positive na mwingine akawa  A negative au B positive na mwingine B negative.Sasa swala ni kwamba watu wa negative wakioana hakuana shida au watu wa positive wakioana hakuna shida LAKINI mwanaume wa positive akioa mwanamke wa negative mtoto wa kwanza atazaliwa vizuri lakini ataacha vitu vinaitwa antibodies ambavyo kazi yake itakua ni kuharibu mimba zote zitakazofuata kutoka kwa mwanaume huyu. Kipimo hichi ni rahisi sana na kinapatikanakaribia hospitali zote Tanzania na hata kama mmeshaoana tayari na mna tatizo hili kuna dawa maalumu inaitwa RHoGAM mama mjamzito anachomwa wiki ya 28 mpaka 32 kuzuia vifo hivyo.
              3.Albinism{Ualbino]: huu ni ugonjwa wa kurithi ambao motto huzaliwa bila vimelea vya melanin au kua na uchache wa vimelea hivyo ambavyo humfanya mtu apate rangi ya ngozi yake. Mara nyingi wazazi wote wawili wa mtoto huyu hubeba ugonjwa huu kwenye miili yao bila kua na dalili yeyote na wao kumzaa mtoto ambaye ni albino lakini pia kuna aina za ualbino ambazo mzazi mmoja anaweza kusababisha albino kuzaliwa bila mama kua na vimelea vya ualibino.Mtoto huyu huzaliwa akiwa na matatizo ya kutoona vizuri na makengeza, ngozi na nywele nyeupe sana. Kua albino sio ugonjwa lakini watu hawa hua kwenye hatari kubwa ya kupata ugonjwa wa kansa ya ngozi. Sio rahisi kupima kujua kama mtu anabeba vimelea vya ualbino kwenye mwili wake lakini inawezekana kupima mtoto aliyeko tumboni na kugundua kama nia albino au sio kwa nchi zilizoendelea au unaweza kumjua mwenzako kwa kuona albino kadhaa kwenye ukoo wao.
              4.Magonjwa ya akili: katika jamii kuna watu hua wanafanya vitu ambavyo sio vya kawaida mpaka unajiuliza huyu mtu amechanganyikiwa au vipi..yaani ni mtu wa fujo, hajifunzi kwa makosa ya nyuma, unasikia mtu kamuua mzazi wake,anavunja sheria mara kwa mara, kunywa pombe sana, anakasirishwa na vitu vidogo sana au maisha yake ya mahusiano yanakua ni ya ugomvi kila siku yaani kwa kifupi anakua tofauti na wengine. Dalili hizi sio za kupuuzia kuna uwezekano mkubwa sana wa kuzaa watoto wa aina hii ambao huanza kusumbua tangu wakiwa shule ya msingi na kupata matatizo makubwa ukubwani. Shida hizi hazihitaji vipimo ni wewe kutoa maamuzi mapema kabla hamjaamua kuzaa naye kwani mambo hayo yanarithiwa na mimi nimeshashuhudia familia nzima ya watu waliokua hawana akili nzuri yaani walikua wehu kabisa.
              5.Magonjwa ya kansa; ugonjwa wa kansa haurithiwi lakini kuna baadhi ya koo zina vimelea{genes] ambazo baadae husababisha kansa. Ni vizuri kujua vyanzo vya vifo vya ndugu wa mwenza wako kabla ya kuamua kuzaa naye kwani ugonjwa huu unaweza kua ni mbaya zaidi kuliko magonjwa yote ya kurithi. Kuna familia naifahamu nyumba ilifungwa kwani watu wote waliuawa na kansa yaani mume na watoto wote waliozaliwa, dada na kaka wote wa mume isipokua mke tu aliyekua ameolewa pale.
              6.Ugonjwa wa kisukari; ugonjwa huu yaani diabetes mellitus type 2 unawapata sana wagonjwa watu wengia ambao kwao kuna ugonjwa huu. Yaani kama baba yako na mama yako wana kisukari uwezekano wa wewe kupata kisukari ni asilimia hamsini. Maana yangu ni kwamba ukioa au ukiolewa na mtu ambao kwao kuna wagonjwa wa kisukari ujue kuna uwezekano wa mtoto wenu mmoja kuugua ugonjwa huo miaka ya baadae. Hivyo hua tunashauri kama wazazi wako wana kisukari kuepuka kua mnene kwani utakikaribisha mapema.
              7.Ugonjwa wa asthma au pumu; ugonjwa huu ambao hushambulia mfumo wa upumuaji hufuata sana ukoo fulani wa watu japokua pumu zipo za aina mbili ile ya kurithiwa na ile ambayo sio ya kurithiwa hivyo kama ukoo unaoenda kuoa au kuolewa una wagonjwa wawili au watatu wa asthma kuna uwezekano mkubwa sana wa kumzaa mtoto mwenye pumu baadae, ugonjwa ambao huua haraka kama usipopata ufuatiliaji wa kutosha.
              8.Ugonjwa wa kifafa; japokua ugonjwa hu huweza kusababishwa na magonjwa mengine kama homa ya uti wa mgongo, ulaji wa nyama ya nguruwe na kadhalika ugonjwa huu umeonekana kufuata koo Fulani za watu yaani kama unaenda kuoa kwenye ukoo ambao unafahamu kuna wagonjwa wa kifafa uwezekano wa kuzaa watoto wenye kifafa upo hivyo ni vema kuingia unajua.
              9.Umbilikimo: huu ni ugonjwa wa kurithi ambao watu wanazaliwa sana kitaalamu unaitwa achondroplasia, wazazi wa watto hawa ambao hua na mikino na miguu mifupi sana huweza kua kawaida kabisa lakini kutokana na kurithi vimelea vya ugonjwa huu hujikuta wanamzaa mtoto huyu na mtoto huyu baada ya muda Fulani akioa anazaa mtoto wa hiv hivi kwani mzazi mmoja tu huweza kusababisha hali hii.
              10.Magonjwa ya upofu; kuna koo ambazo watoto huzaliwa na vimelea vya hali ambayo husababisha upofu baadae au ikasababisha upofu hata kabla ya mtoto kufikisha miaka mitano. Mtoto huzaliwa na mtoto wa jicho kitaalamu kama congenital cataract ambayo huziba jicho taratibu na baadae mtu hataona kabisa na unaweza ukakuta ukoo una vipofu wengi na chanzo husika hakifahamiki.
              Mwisho; haya ni baadhi ya magonjwa tu ambayo labda yameathiri watu wengi kwenye jamii zetu lakini yapo mengine mengi ambayo siwezi kuyataja na  makala hii haijaandikwa kuwatenga au kuwasema vibaya watu wenye matatizo haya kwamba wasioe au wasiolewe lakini ni kujaribu kuongea ukweli na kuepusha watu wenye tatizo moja kuzaa mtoto kwani ni kujiongezea matatizo tu kama nilivyosema hapo mwanzoni na kuleta viumbe ambavyo vinakuja duniani kuteseka sana. Ni bora waendelee kuzaliwa carriers yaan wanaobeba vimelea bila kuugua kuliko kuendelea kuwazaa wagonjwa.hivyo kama wewe unajua kwenu kuna shida fulani ni bora kuzaa na mtu ambaye kwao hamna shida kabisa kwani ukizaa na mtu mwenye matatizo kwao pia ni hatari zaidi na kama ukiamua kukaidi na  kuzaa hivyohivyo uzae unajua kwamba haya magonjwa yapo. niwape pole ambao tayari ni wagonjwa wa hali hizi na wale wenye ndugu wenye hali hizi.dunia inatambua maumivu yenu...